RAIS DKT. SAMIA KUFUNGUA MKUTANO MKUBWA WA MADINI NOVEMBA 2026
RAIS DKT. SAMIA KUFUNGUA MKUTANO MKUBWA WA MADINI NOVEMBA 2026
▪️ Ni Mkutano mkubwa wa Madini na Uwekezaji ▪️Washiriki 2000 kutoka mataifa 50 Duniani kushiriki ▪️Kauli Mbiu ya Mkutano inalenga kuongeza thamani madini kwa maendelezo ya Viwanda ▪️Serikali na Sekta Binafsi kushirikiana kuandaa mkutano huo ▪️Waziri Mavunde azindua rasmi maandalizi ya mkutano huo 📍 DAR ES SALAAM. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia S. Hassan anatarajiwa kufungua rasmi Mkutano wa Saba wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIC 2026) utakaofanyika Novemba 19 hadi 21, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Akizungumza leo Juni 27, 2026 wakati wa uzinduzi wa TMIC 2026, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema serikali imeamua kujenga uchumi wa viwanda unaotokana na madini kwa kuwekeza katika uchakataji na uyeyushaji wa madini badala ya kuendelea kuuza malighafi. Amesema kaulimbiu ya mkutano huo, "Madini Yaliyoongezwa Thamani: Chachu ya Ukuaji wa Viwanda na Uchumi," inaakisi dira ya serikali ya kuifanya Ta…