PSSSF YAASA WABUNGE KUIFANYA SEKTA YA NGOZI KUWA MWAMBA WA VIWANDA NA AJIRA NCHINI

PSSSF YAASA WABUNGE KUIFANYA SEKTA YA NGOZI KUWA MWAMBA WA VIWANDA NA AJIRA NCHINI
Na Dotto Kwilasa, Dodoma Katika harakati za kukuza uchumi wa viwanda nchini, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umehimiza Wabunge kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya bidhaa za ngozi zinazozalishwa ndani ya Tanzania, hatua inayolenga kuimarisha viwanda vya ndani, kuongeza ajira na kukuza thamani ya rasilimali za taifa. Akizungumza Juni 15, 2026 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Fortunatus Makore Magambo alieleza kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya kujenga uchumi imara kupitia sekta ya ngozi, endapo bidhaa zake zitapata soko la kutosha la ndani na nje ya nchi. Akiwasilisha taarifa ya shughuli na mafanikio ya Kiwanda cha Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited (KLICL), Magambo alisema uwekezaji uliofanyika katika sekta hiyo tayari umeanza kuleta matokeo chanya kwa kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na kuimarisha mnyororo wa uzalishaji wa viwanda. Amesema sekta ya ngozi ni miongoni mwa maene…