Profesa Mbarawa: Mabaharia ni Nguzo ya Uchumi na Usafirishaji Duniani

Profesa Mbarawa: Mabaharia ni Nguzo ya Uchumi na Usafirishaji Duniani
-Asilimia 80 ya Mizigo Inaingia Tanzania Kwa Njia ya Maji NA MWANDISHI WETU, KIGOMA WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amesema mabaharia ni nguzo muhimu ya usafirishaji duniani na walinzi wakuu wa mnyororo wa biashara na uchumi, hivyo wanapaswa kuendelea kupewa mazingira bora ya kazi, mafunzo na fursa za maendeleo ili kuongeza mchango wao katika uchumi wa taifa. Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 16  Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika mkoani Kigoma. Alisema zaidi ya asilimia 80 ya biashara ya dunia husafirishwa kwa njia ya maji, jambo linalowafanya mabaharia kuwa mhimili muhimu wa uchumi wa kimataifa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwemo kukaa muda mrefu baharini, kutengana na familia zao, mazingira magumu ya kazi na hatari za kiusalama, bado wanaendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kujitolea. “Mabaharia ndio uti wa mgongo wa sekta ya usafirishaji duniani. Kazi yao inahakikisha bidhaa muhimu zi…