PROF. SHEMDOE AWATAKA WALIMU KUONGEZA UBUNIFU KATIKA UFUNDISHAJI

PROF. SHEMDOE AWATAKA WALIMU KUONGEZA UBUNIFU KATIKA UFUNDISHAJI
Walimu 35 walioshinda tuzo za ufundishaji kupatiwa viwanja WALIMU nchini wamehimizwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kutumia mbinu bunifu za ufundishaji ili kuimarisha ubora wa elimu na kuchangia maendeleo ya taifa. Aidha, walimu 35 walioibuka washindi katika Shindano la Taifa la Stadi za Ufundishaji wameelekezwa kupatiwa viwanja karibu na maeneo yao ya kazi kama sehemu ya motisha. Akizungumza Juni 6, 2026 jijini Dar es Salaam katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano hilo kwa walimu wa elimu ya awali, msingi na sekondari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amesema walimu wana mchango mkubwa katika kuwalea na kuwaandaa wanafunzi kuwa wananchi wenye maarifa, stadi na maadili mema yanayohitajika katika jamii. Prof. Shemdoe amesema Serikali itaendelea kuthamini mchango wa walimu kwa kuweka mazingira bora ya kazi pamoja na motisha mbalimbali zinazolenga kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, amewataka walimu …