PROF. SHEMDOE AELEKEZA MAAFISA UTUMISHI WALIOKWAMISHA WATUMISHI KUPANDA MADARAJA KUCHUKULIWA HATUA
• Aelekeza kijana mlemavu Joseph kupewa ajira ya kudumu Na OWM - TAMISEMI, Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amemuelekeza Katibu Mkuu - UTUMISHI Bw. Juma Selemani Mkomi kufanya tathmini ya kubaini Maafisa Utumishi waliozembea kukamilisha mchakato wa Watumishi wa Umma kupandishwa madaraja kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kuwachukulia hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma. Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo Juni 23, 2026 kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026 katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma. “Kuna Maafisa Utumishi kwa uzembe wamesababisha watumishi kutopandishwa madaraja mwaka 2025/26, Katibu Mkuu UTUMISHI kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi nakuelekeza kufanya tathmini ya kubaini maafisa waliokwamisha upandishaji wa madaraja na kuchukua hatua …