POLISI WAFICHUA MPANGO WA UHALIFU JULAI 7

POLISI WAFICHUA MPANGO WA UHALIFU JULAI 7
Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa watu wote wanaohamasisha na kupanga kutekeleza vitendo vya uvunjifu wa amani na uhalifu nchini, wakiwemo wale wanaochochea kufanyika kwa maandamano mnamo tarehe 7 Julai mwaka huu. Onyo hilo limetolewa kufuatia kuwepo kwa maswali mengi kutoka kwa baadhi ya wananchi hivi karibuni, wakitaka kujua jinsi jeshi hilo linavyofuatilia na kushughulikia uhamasishaji huo wa uvunjifu wa amani unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu kupitia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii. Kupitia taarifa yake, Jeshi la Polisi limesema linafuatilia kwa karibu sana shughuli hizo zote kupitia mifumo yake mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii, ambapo imegundulika kuwa watu hao wameacha ajenda ya awali ya maandamano yasiyozingatia sheria na sasa wanahamasishana kufanya vitendo vizito vya kihalifu. Miongoni mwa vitendo vya hatari vinavyohamasishwa ni pamoja na kufunga barabara, kuchoma moto shule kwa lengo la kusababisha taharuki kwa wazazi na walezi, kushambulia wananchi,…