Picha : CHEREHANI AZINDUA SHULE YA A-LEVEL SABASABINI USHETU

Picha : CHEREHANI AZINDUA SHULE YA A-LEVEL SABASABINI USHETU
Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini (Kidato cha Tano na Sita) iliyopo Kata ya Sabasabini, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.  Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani (aliyevaa miwani), akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini, uliofikia hatua za mwisho za ukamilishaji na unatarajiwa kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu ya sekondari. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog, Ushetu Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani, amezindua rasmi Shule ya Sekondari ya Juu Sabasabini (Kidato cha Tano na Sita) iliyopo Kata ya Sabasabini, huku akiipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha sekta ya elimu na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo ya vijijini. Uzinduzi huo…