ORYX GAS ,KIDOTI FOUNDATION KUWAWEZESHA MITUNGI YA GESI WATOA HUDUMA ZA SALUNI

ORYX GAS ,KIDOTI FOUNDATION KUWAWEZESHA MITUNGI YA GESI WATOA HUDUMA ZA SALUNI
Na Mwandishi Wetu. KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania kwa kushirikana na taasisi ya Kidoti Foundation wameingia makubaliano ya kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini kwa kulifiki kundi la watoa huduma za Saluni nchini. Kwa mujibu wa Oryx na Kidodi Foundation watoa huduma za Saluni nchini ni kundi lenye uwezo mkubwa wa kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kutokana na mwingiliano wao wa karibu na jamii, hali inayowafanya kuwa mabalozi muhimu wa mabadiliko ya tabia na mtazamo kuhusu matumizi ya nishati hiyo. Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa Kidoti Foundation, Jokate Mwegelo, ambaye pia ni mlezi wa Chama cha Salunisti Tanzania (CCST) amesema lengo la kuwawezesha watoa huduma za saluni kutumia nishati safi na kuwa mabalozi wa kuhamasisha matumizi yake katika jamii. Amesema kundi la wasusi na watoa huduma za saluni lina nafasi ya kipekee kwa kuwa hukutana na mamia ya wananchi kila siku, jambo linaloweza kutumiwa kue…