NEMC YATAMBUA SHULE BORA ZA UHIFADHI WA MAZINGIRA: SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI
NEMC YATAMBUA SHULE BORA ZA UHIFADHI WA MAZINGIRA: SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa tuzo na vyeti kwa shule za Msingi zinazofanya vizuri katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira katika Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kimkoa Juni 5, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, yakiongozwa na kauli mbiu isemayo, “Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.” Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi na usimamizi wa mazingira ili kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Amesema utunzaji wa mazingira ni msingi muhimu wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku akisisitiza umuhimu wa kuwajengea vijana na wanafunzi utamaduni wa kulinda mazingira tangu wakiwa wadogo. “Tunahitaji kuongeza juhudi za pamoja katika kulinda mazingira yetu, kwani mafanikio ya Dira 2050…