NCHIMBI MGENI RASMI SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2026 DODOMA
NCHIMBI MGENI RASMI SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2026 DODOMA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajia kuwa mgeni rasmi Siku ya Mazingira Duniani (WED) 2026 akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, ambapo kitaifa yatafanyika Juni 5, 2026 jijini Dodoma katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC) jijini Dodoma. Hayo yamesema Juni 4, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, alipotembelea mabanda ya maonesho ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku. Mhe, Masauni ametoa wito kwa sekta zote nchini kuimarisha juhudi za utunzaji na uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 yanafikiwa kwa ufanisi. Amesema kuwa utunzaji wa mazingira ni ajenda ya kitaifa inayohitaji ushiriki wa kila sekta ya uchumi na si jukumu la taasisi au wizara moja pekee, akisisitiza kuwa maendeleo endelevu hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa maz…