Nchi Zinazolima Tumbaku Zaungana Kulinda Zao Linalochangia Uchumi wa Mamilioni
Nchi Zinazolima Tumbaku Zaungana Kulinda Zao Linalochangia Uchumi wa Mamilioni
Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam Tanzania imesisitiza umuhimu wa zao la tumbaku kwa uchumi wa nchi kubwa zinazolizalisha barani Afrika, ikitoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano wa kikanda ili kulinda maisha ya mamilioni ya wakulima na kuhakikisha sera za kimataifa kuhusu tumbaku zinazingatia hali halisi ya nchi zinazozalisha zao hilo. Akifungua mkutano wa nchi zinazolima tumbaku uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, alisema tumbaku inaendelea kuwa zao muhimu la kimkakati kutokana na mchango wake mkubwa katika upatikanaji wa fedha za kigeni, ajira, mapato ya Serikali, maendeleo ya viwanda na kupunguza umaskini. "Kwa nchi zetu, tumbaku si zao la kawaida bali ni bidhaa ya kimkakati inayochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya uchumi," alisema Chongolo, akisisitiza kuwa sera za kimataifa zinazoihusu sekta hiyo zinapaswa kuzingatia ushahidi wa kisayansi na tathmini halisi ya athari zake kiuchumi na kijamii kwa nchi zinazozalisha. Al…