NAIBU WAZIRI MWIJUMA AITAKA SEKTA YA FEDHA KUWA CHACHU YA MAENDELEO YA JAMII
NAIBU WAZIRI MWIJUMA AITAKA SEKTA YA FEDHA KUWA CHACHU YA MAENDELEO YA JAMII
Na Oscar Assenga, Tanga Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma (MB), amesisitiza umuhimu wa taasisi za kifedha nchini kuendelea kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii kwa kuanzisha na kuunga mkono mipango inayolenga kuboresha maisha ya wananchi. Akizungumza jijini Tanga wakati wa uzinduzi rasmi wa ushirikiano kati ya Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kupitia mpango wa “Cash Waqf”, Mwinjuma alisema ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuongeza upatikanaji wa rasilimali fedha za kufadhili elimu ya juu nchini. Uzinduzi huo pia uliambatana na ufunguzi rasmi wa tawi la PBZ IKHLAS, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo wa kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi. “Ni muhimu taasisi za fedha nchini kuendelea kushiriki katika maendeleo ya jamii kwa kuunga mkono mipango itakayowanufaisha wananchi katika maeneo mbalimbali,” alisema Mwinjuma. Aidha, aliipongeza PBZ kwa juhudi zake za kupanu…