MWENYEKITI UWT PWANI AUNGURUMA KIBAHA MJI AWAHIMIZA WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI
MWENYEKITI UWT PWANI AUNGURUMA KIBAHA MJI AWAHIMIZA WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Na Victor Masangu,Kibaha Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu amewahimiza wanawake kuweka misingi imara ya kutumia fursa za mikopo ya asilimia 10 ambayo inatolewa na Hamashauri kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini. Vullu ameyabainisha hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambapo ameweza kutembelea katiika kata mbili za Tumbi pamoja na Kata ya Kongowe ambapo ameambatana na kamati ya utekelezaji ya Mkoa pamoja na vingozi ngazi ya Wilaya. Katika ziara hiyo Mwenyekiti huyo ameweza kupata fursa ya kutembelea baadhi ya miradi ikiwemo katika sekta ya elimu ambapo ameweza kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa choo salama katika wa sekondari ya Kibaha pamoja na kituo cha afya Kongowe. Mwenyekiti huyo amesema kwamba lengo kubwa la kufanya ziara hiyo ni kwa ajili ya kuwashukuru umoja wa wanawake UWT kwa kuweza kuwa pamoja na mshikamano wa kukiwezesha chama cha mapinduzi kuweza kushi…