MUHEZA YAJIPANGA KUNG’ARA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2026

MUHEZA YAJIPANGA KUNG’ARA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2026
Na Mwandishi Wetu, Muheza Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Ayoub Sebabili, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika shughuli za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2026, akisema ushiriki mkubwa wa wananchi utasaidia wilaya hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya Kitaifa ya Mwenge wa Uhuru. Sebabili ametoa wito huo wakati wa zoezi la Jogging lililoandaliwa kama sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, ambapo aliwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki shughuli hiyo. Alisema Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili wilayani Muheza Juni 23, 2026 ukitokea Wilaya ya Mkinga na kupokewa katika eneo la Kilapura, huku ukitarajiwa kulala katika Uwanja wa Jitegemee. “Niwashukuru kwa namna mlivyojitokeza leo. Ushiriki wenu unaonyesha dhamira ya kuhakikisha Muheza inafanya vizuri katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru. Kila mmoja wetu awe balozi wa kuhamasisha wananchi wengine kujitokeza kwa wingi,” alisema Sebabili.. Kwa upande wake, Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Muhe…