MUHAS YAWAKUTANISHA WANASAYANSI KUJADILI USUGU WA VIMELEA DHIDI YA DAWA, WAHIMIZA MATUMIZI SAHIHI YA ANTIBIOTIKI
MUHAS YAWAKUTANISHA WANASAYANSI KUJADILI USUGU WA VIMELEA DHIDI YA DAWA, WAHIMIZA MATUMIZI SAHIHI YA ANTIBIOTIKI Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Maalum ya Kitaifa ya Kupambana na Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa, Profesa Hezron Nonga, a kifungua Kongamano la Kisayansi la kujadili na kuwasilisha matokeo ya tafiti kuhusu usugu wa vimelea dhidi ya dawa lililofanyika Juni 3, 2026, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dar es Salaam. Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Erasto Mbugi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano la Kisayansi kuhusu usugu wa vimelea Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili ya Microbiology MUHAS, Lilian Kiwone akieleza umuhimu wa kushiriki Kongamano la Kisayansi kuhusu usugu wa vimelea. ………… NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimeandaa Kongamano la Kisayansi linalolenga kujadili na kuwasilisha matokeo ya tafiti kuhusu usugu wa vimelea dhidi ya dawa kwa binadamu na wanyama pamoja na uhamasisha ufugaji wa kisasa unaozingatia usafi wa mazingira ya mifugo ili kup…