Msajili wa Hazina aonya taasisi za umma zenye utendaji duni

Msajili wa Hazina aonya taasisi za umma zenye utendaji duni
Serikali imeonya taasisi za umma zinazofanya vibaya kujitathmini na kuchukua hatua za haraka za kuboresha utendaji wao, ikisisitiza kuwa haitavumilia taasisi zitakazoendelea kuonesha utendaji duni kwa muda mrefu. Onyo hilo lilitolewa na Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, jijini Dar es Salaam Ijumaa, Juni 26, 2026, wakati wa mahojiano maalumu kuelekea Siku ya Gawio itakayofanyika Jumanne, Juni 30, 2026, katika Ikulu ya Dar es Salaam. Bw. Mchechu alisema taasisi zote zinazostahili kuwasilisha gawio na michango mingine Serikalini zinapaswa kutekeleza wajibu huo kwa wakati, akisisitiza kuwa kushindwa kufanya hivyo ni kuinyima Serikali na wananchi mapato stahiki. “Mashirika si mali ya bodi za wakurugenzi wala menejimenti; ni mali ya umma zinazosimamiwa na Serikali. Kwa muktadha huo, kurejesha kilicho haki ya wananchi si fadhila, bali ni wajibu,” alionya. Alisisitiza kuwa viongozi wa taasisi za umma wanapaswa kuhakikisha malengo ya faida wanayopewa yanafikiwa ili kuongeza mchango wa taasi…