MRADI WA KUJENGA UHIMILIVU DHIDI YA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KIGOMA WAFIKIA HATUA MUHIMU
MRADI WA KUJENGA UHIMILIVU DHIDI YA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KIGOMA WAFIKIA HATUA MUHIMU Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ufadhili wa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) kwa kushirikiana na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), imefikia hatua muhimu katika utekelezaji wa Mradi wa Kujenga Uhimilivu dhidi ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Mkoa wa Kigoma kwa kuanza uthibitishaji wa matokeo ya tathmini ya awali ya mradi huo. Uthibitishaji huo unafanyika kupitia warsha iliyofanyika katika Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma Juni 26, 2026 ukilenga kuhakiki hali halisi ya kijamii, kiuchumi na kimazingira katika maeneo ya mradi kabla ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kuimarisha uhimilivu wa jamii dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Meneja wa Mradi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Onesphory Kamukuru alisema mradi unatekelezwa katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko kutokana na maeneo hayo kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na uharib…