MKAKATI MPYA WA SEZS: TANZANIA YATENGA MAENEO MAALUM YA UWEKEZAJI NA KUONGEZA ULINZI WA ARDHI

MKAKATI MPYA WA SEZS: TANZANIA YATENGA MAENEO MAALUM YA UWEKEZAJI NA KUONGEZA ULINZI WA ARDHI
Na Janeth Raphael MichuziTv- Bungeni Dodoma Serikali ya Tanzania imeeleza mkakati wake wa kuendeleza na kutenga Maeneo Maalum ya Uwekezaji (Special Economic Zones – SEZs) kwa lengo la kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, kupitia uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na miundombinu wezeshi. Hayo yameelezwa Bungeni na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt.Pius Chaya alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Itigi, Yohana Stephen Msita, aliyehoji kuhusu hatua za Serikali katika kutenga ardhi na kulipa fidia kwa ajili ya maeneo hayo ya uwekezaji. Dkt. Chaya amebainisha kuwa Serikali, kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), inaendelea kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kutambua, kutenga na kuendeleza maeneo ya kimkakati ya uwekezaji kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali. Taasisi hizo ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI pamoja na Ofisi ya Msajili wa Hazina. Ushirikiano h…