MIAKA TISA YA SuFP YAVUTA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO KARIBU NA WANANCHI
MIAKA TISA YA SuFP YAVUTA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO KARIBU NA WANANCHI
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV MKURUGENZI Muendeshaji wa shirika lisilo la kiserikali (MSI) Tanzania, Dkt. Stephen Mutegeki, amesema utekelezaji wa Programu ya Scaling Up Family Planning (SuFP) kwa kipindi cha miaka tisa umechangia kwa kiasi kikubwa kusogeza huduma za afya ya uzazi na uzazi wa mpango karibu na wananchi, hususan wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na makundi mengine yaliyokuwa magumu kufikiwa. Dkt. Mutegeki ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa Kongamano la Kujifunza la Programu ya SuFP lililofanyika chini ya kaulimbiu isemayo, “Kudumisha Mafanikio Yaliyopatikana katika Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango.” Amesema MSI Tanzania, kama mmoja wa washirika wa utekelezaji wa programu hiyo iliyofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Foreign, Commonwealth and Development Office (FCDO), imejikita katika kuimarisha mifumo ya afya ya umma, kuboresha ubora wa huduma na kujenga uwezo wa wataalamu wa afya ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi wengi zaidi. Kwa mujibu w…