MCHENGERWA ATEMA CHECHE NZITO UFUNGUZI WA MAFUNZO YA MADIWANI WA CCM PWANI

MCHENGERWA ATEMA CHECHE NZITO UFUNGUZI WA MAFUNZO YA MADIWANI WA CCM PWANI
Na Victor Masangu, Kibaha Madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani wametakiwa kujenga mising imara iya kuwa na uzalendo na Taifa lao ikiwa  pamoja na kuweka mikakati  kabambe ya kupambana na kero na chanagamoto mbali mbali za wananchi ili kuweza kuzitafuta ufumbuzi. Hayo yamebainishwa na  Mjumbe wa halmashauri kuu ya (CCM) Taifa  Mohamed Mchengerwa (MNEC)  ambaye pia ni  Waziri wa afya wakati   wa kufungua mafunzo maalumu kwa madiwani wa CCM Mkoa wa Pwani  ambayo yamefanyika katika shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere iliyopo eneo la kwa mfipa katika  Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani. Mchengerwa amesema kwamba  mafunzo hayo  kwa madiwani wa Mkoa wa Pwani  watawajengea uwezo mkubwa katika suala zima  la kuwatumikia wananchi wao ikiwemo kusikiliza kero na  changamotto mbali mbali ambazo  zinawakabili  wanapaswa kuwa wazalendo. Kadhalika Mchengerwa amesema kwamba madiwani wanapaswa kuabdilika na kuwa mstari wa mbele katika kwenda  kuwa suluhisho  katika  kuwas…