MBUNGE WA KALENGA JACKSON KISWAGA AIBANA SERIKALI KUHUSU UJENZI WA BARABARA YA IFUNDA–KIPONZERO
NA DENIS MLOWE IRINGA MBUNGE wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga, ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kusimamia maendeleo ya wananchi kwa kuibana Serikali kuhusu hatima ya ujenzi wa barabara ya Ifunda–Kiponzero yenye urefu wa kilomita 12, ambayo ni muhimu kwa shughuli za kiuchumi na kijamii katika eneo hilo. Akiuliza swali la nyongeza bungeni, Mheshimiwa Kiswaga alisema barabara hiyo ni kiungo muhimu kinachorahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa katika maeneo ya Ifunda na Kiponzero, hivyo alihoji ni lini Serikali itaona umuhimu wa kuijenga kwa kiwango cha lami ili kuongeza kasi ya maendeleo ya uchumi kwa wananchi wa Kalenga. “Barabara ya kutoka Ifunda kwenda Kiponzero ni barabara muhimu sana ya kiuchumi. Je, ni lini sasa Serikali, maana ni kilomita 12 tu, itaona umuhimu wa kutujengea kwa lami ili tuendelee kuchagiza shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika eneo hilo?” alihoji Mbunge huyo. Akijibu swali hilo kwa niaba ya Serikali,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa n…