MAZISHI YA MAMA MZAZI WA MHANDISI JAMES JUMBE KUFANYIKA KESHO JUMATANO

MAZISHI YA MAMA MZAZI WA MHANDISI JAMES JUMBE KUFANYIKA KESHO JUMATANO
Mhandisi James Jumbe Wiswa akiwa katika picha ya kumbukumbu na mama yake mzazi, marehemu Magreth Limbe Mwinula, enzi za uhai wake. Mama Magreth amefariki dunia na anatarajiwa kuzikwa Juni 10, 2026.  **** Mazishi ya Magreth Limbe Mwinula, mama mzazi wa Mhandisi James Jumbe Wiswa, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Juni 10, 2026, katika eneo la Mwasele-Matenkini mkoani Shinyanga. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na familia, shughuli za mazishi zitaanza majira ya asubuhi kwa ibada ya kuaga mwili nyumbani Majengo ya Zamani Mjini Shinyanga kabla ya mwili wa marehemu kupelekwa katika Kanisa la Moyo Safi wa Maria, Shinyanga Mjini kwa ajili ya ibada ya mazishi. Baada ya ibada hiyo, mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda eneo la mazishi ambapo ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kabla ya maziko kufanyika. Magreth Limbe Mwinula alifariki dunia Juni 4, 2026 akiwa na umri wa miak…