MAKUBALIANO MANANE: RAMANI MPYA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI TANZANIA NA URUSI YAFUNULIWA

Na Mwandishi Wetu, TBN, Dar es salaam Mikataba na hati za makubaliano manane (8) zilizosainiwa kati ya Tanzania na Urusi, ndizo zilizoweka msingi mkuu wa ushirikiano mpya wa kiuchumi, kijamii na kiteknolojia unaotarajiwa kupandisha hadhi ya nchi hizi mbili.  Makubaliano haya makubwa, ambayo ni matunda ya moja kwa moja ya ziara ya kihistoria ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi, yanajenga daraja imara la maendeleo katika sekta tisa za kipaumbele: kilimo, elimu, nishati, madini, viwanda, utalii, usafirishaji, uchumi wa kidijiti, pamoja na biashara na uwekezaji. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, ameanika hadharani undani wa makubaliano hayo manane yanayobeba mustakabali wa nchi: Kutoka Diplomasia ya Lugha Hadi Mapinduzi ya Afya na Elimu ya Juu Katika makubaliano ya kwanza, Tanzania na Urusi zimeamua kutumia lugha kama silaha ya kidiplomasia. Kupitia hati ya ushirikiano kati ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Chuo Kikuu cha Mahusiano ya Ki…