KWA NINI CHEREHANI ANASEMA MEMA YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA USHETU HAYAWEZI KUELEZWA KWA SIKU MOJA?

KWA NINI CHEREHANI ANASEMA MEMA YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA USHETU HAYAWEZI KUELEZWA KWA SIKU MOJA?
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani **** Kauli ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, kwamba "Mafanikio ya Rais Samia Ushetu hayawezi kuelezeka kwa siku moja" inaweza kuonekana kama kauli ya kawaida ya kisiasa.  Hata hivyo, ukiichambua kwa kina na kuangalia kiwango cha uwekezaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika Jimbo la Ushetu, unagundua kuwa kauli hiyo imejengwa juu ya miradi halisi ya maendeleo inayoonekana kwa macho. Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa Jengo jipya la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu lililopo Nyamilangano, Cherehani alisema mchango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maendeleo ya jimbo hilo ni mkubwa kiasi kwamba ni vigumu kuueleza kwa siku moja. Kwa mtazamo wa kisiasa na maendeleo, hoja ya Cherehani inapata nguvu kutokana na takwimu na miradi iliyotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka michache ya uongozi wa Rais Samia. Muonekano wa Jengo jipya la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu …