KUTOKA TAKA HADI HAZINA: SAFARI YA TRASH TO TREASURE INAYOBADILISHA MAISHA

KUTOKA TAKA HADI HAZINA: SAFARI YA TRASH TO TREASURE INAYOBADILISHA MAISHA
“Taka ni mali.” Hiyo si kauli mbiu tu kwa Trash to Treasure iliyopo Sumbawanga, mkoani Rukwa. Ni maisha, ni imani, na ni safari iliyoanza kutoka kwenye kumbukumbu za utoto. Mwanzilishi wa Trash to Treasure anatoka katika familia ya kipato cha chini. Akiwa mtoto, mazingira ya kujifunzia hayakuwa rahisi. Vifaa vya kujifunzia vilikuwa vichache, na mara nyingi yeye na watoto wengine walitumia vijiti, vizibo vya soda na vitu vya kawaida vilivyopatikana mazingira ya karibu kama njia ya kujifunzia na kucheza. Lakini kulikuwa na jambo lingine lililomgusa zaidi. Kila jioni baada ya shule, yeye na marafiki zake walikuwa wakielekea uwanjani kucheza mpira huku kila mmoja akiwa na ndoto ya kuwa kama Ronaldo. Karibu na uwanja huo kulikuwa na mto mdogo. Kila mvua iliponyesha, maji yalifurika yakiwa yamebeba taka nyingi za plastiki. Maji hayo yaliingia mpaka uwanjani, yakiacha uchafu kila mahali. Kwa mtoto mdogo, hiyo ilikuwa kero. Lakini miaka kadhaa baadaye, jambo lile lile ambalo lilionekana kuwa tatizo lilianza …