KITUO CHA KUBADILISHIA UMEME MBANDE KUIMARISHA UHAKIKA WA UMEME KONGWA NA WILAYA JIRANI
KITUO CHA KUBADILISHIA UMEME MBANDE KUIMARISHA UHAKIKA WA UMEME KONGWA NA WILAYA JIRANI Na. Meleka Kulwa – Fullshangwe Blog, Dodoma Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amezindua Kituo cha Kubadilishia Njia za Usambazaji Umeme (Switching Station) pamoja na transfoma ya kudhibiti umeme kilichopo Mbande, wilayani Kongwa, mkoani Dodoma. Akizungumza Juni 16, 2026 katika uzinduzi huo, Waziri Ndejembi amesema kuwa mradi huo unalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuongeza ufanisi wa mfumo wa usambazaji na kuboresha huduma kwa wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Kongwa na wilaya jirani. Aidha, amebainisha kuwa kukamilika kwa miundombinu hiyo kutaimarisha huduma ya umeme katika wilaya za Kongwa, Gairo, Chamwino na baadhi ya maeneo ya wilaya za Mpwapwa na Kiteto. Pia amesema kuwa miundombinu hiyo itaongeza uthabiti wa mfumo wa usambazaji umeme, kupunguza athari za hitilafu, kuboresha viwango vya umeme na kuongeza uwezo wa TANESCO kuhudumia mahitaji ya sasa na ya baadaye ya wananchi na wawekezaji. Ameongeza kuwa Serikali inatarajia kuona ongeze…