KIPANGULA: KUKOSOA NI NGUZO YA DEMOKRASIA, SIYO KOSA
KIPANGULA: KUKOSOA NI NGUZO YA DEMOKRASIA, SIYO KOSA
Na Mwandishi Wetu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema kuwa kukosoa ni haki ya msingi katika jamii ya kidemokrasia, lakini ukosoaji huo unapaswa kufanywa kwa kuzingatia maadili, heshima na ukweli. Akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Barnabas Lucas, baada ya kuwasilisha mada kuhusu “Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Enzi ya Kidijiti: Wajibu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari” katika Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari lililoandaliwa na UDOM kupitia Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari. Wakili Kipangula amezungumza mipaka ya uhuru wa kujieleza na ukosoaji wa viongozi katika jamii. Amesisitiza kuwa wananchi wana haki ya kutoa maoni na kukosoa, lakini wanapaswa kufanya hivyo kwa lugha yenye staha na inayojenga. “Kukosoa siyo kosa, lakini kukosoa siyo kutukana. Kukosoa siyo kubagua, na kukosoa siyo kudhalilisha. Tunapaswa kutofautisha kati ya kutoa hoja za kujenga na …