KIPANGULA AWATAKA WAANDISHI KUIPA HADHI TAALUMA YA HABARI

Na Mwandishi Wetu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amewashauri Waandishi wa Habari nchini kuipa thamani na heshima taaluma ya habari kwa kuzingatia nadhifu ya mavazi na mienendo yao wanapotekeleza majukumu ya kitaaluma. Wakili Kipangula ametoa ushauri huo leo Juni 5, 2026 wakati akiwasilisha mada kuhusu “Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Enzi ya Kidijiti: Wajibu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari” kwenye Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari. Amesema uandishi wa habari ni taaluma muhimu inayotambulika kama muhimili wa nne usio rasmi katika jamii, hivyo ni wajibu wa waandishi wenyewe kuhakikisha wanaijengea heshima kupitia mwenendo, maadili na namna wanavyojiwasilisha mbele ya jamii. Wakili Kipangula amesema mwonekano wa mwandishi wa habari unaweza kuwa sehemu ya kujenga imani kwa jamii na vyanzo vya habari vinavyotoa taarifa …