KARIBU- KILIFAIR NI UWEKEZAJI WA KIMKAKATI AMBAO TANAPA HUUTUMIA KUNADI VIVUTIO VYAKE VYA UTALII .
KARIBU- KILIFAIR NI UWEKEZAJI WA KIMKAKATI AMBAO TANAPA HUUTUMIA KUNADI VIVUTIO VYAKE VYA UTALII .
Na. Calvin Katera - Arusha. Maonesho ya Karibu- KiliFair yameendelea kuwa na umuhimu mkubwa kwa TANAPA kwani ni jukwaa la kuwakutanisha wadau wa ndani na nje ili kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika Hifadhi za Taifa nchini. Kupitia maonesho hayo, TANAPA hukutana na wadau mbalimbali wa utalii wa ndani na nje ambao wameendelea kuwekeza na kuchagiza ongezeko la watalii katika Hifadhi za Taifa nchini. Akifungua Maonesho hayo leo juni 05, 2026 katika Viwanja vya Magereza jijini Arusha, Mkurugenzi wa Utalii Dkt. Thereza Mugobi kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alisema kuwa Karibu-KiliFair ni zaidi ya maonesho, vilevile ni uwekezaji wa kimkakati katika mustakabali wa utalii wa Tanzania. Uhusiano huu wa kibiashara ulioanzishwa katika jukwaa hili la Karibu KiliFair umezalisha ushirikiano mpya, kuongeza idadi ya watalii wanaowasili nchini, kuvutia uwekezaji, kutengeneza ajira, na kuimarisha maisha ya jamii zinazotegemea utalii. "Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombi…