KAPINGA: DHANA YA TAKA SIFURI INAFUNGUA FURSA ZA BIASHARA NA VIWANDA.
KAPINGA: DHANA YA TAKA SIFURI INAFUNGUA FURSA ZA BIASHARA NA VIWANDA.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema dhana ya taka sifuri na urejeshaji bidhaa ni fursa muhimu ya kukuza sekta ya viwanda, kuongeza thamani ya malighafi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza katika kikao cha mawaziri kilichofanyika jijini Istanbul nchini Uturuki, Juni 5, 2026, kilichobeba mada ya Mageuzi ya Kijani ya Viwanda: Mtazamo wa taka sifuri na urejeshaji bidhaa, Kapinga amesema Tanzania inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta ya viwanda huku ikisisitiza matumizi bora ya rasilimali na uhifadhi wa mazingira. Ameeleza kuwa dhana ya taka sifuri na urejeshaji bidhaa inatoa fursa kwa nchi zinazoendelea kupitia matumizi endelevu ya malighafi, kupunguza upotevu baada ya mavuno, kupunguza uzalishaji wa taka na kuongeza thamani ya bidhaa zinazotengenezwa viwandani. Kapinga amesema Serikali ya Tanzania imeendelea kuunganisha masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika sera na mipango ya maendeleo ya viwanda kwa kuha…