KAMPUNI YA PRO FLIGHT LTD HELICOPTERS  TANZANIA -KENYA YAANZA SAFARI ZAKE ARUSHA

KAMPUNI YA PRO FLIGHT LTD HELICOPTERS  TANZANIA -KENYA YAANZA SAFARI ZAKE ARUSHA
Afisa wa Udhibiti wa Ubora na Usalama wa kampuni hiyo, Julius Ngeno akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha  Happy Lazaro,Arusha . Arusha .Wakati maelfu ya wadau wa utalii kutoka ndani na nje ya Tanzania wakikutana katika Maonesho ya Kimataifa ya Karibu-KiliFair jijini Arusha, teknolojia ya usafiri wa anga imeendelea kujitokeza kama moja ya suluhisho muhimu katika kurahisisha huduma kwa watalii na wasafiri wanaotembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii. Miongoni mwa washiriki waliovutia macho ya wadau katika maonesho hayo ni kampuni ya usafiri wa anga ya Pro Flight Ltd Helicopters Tanzania -Kenya, ambayo imekuja na huduma za kisasa za helikopta zinazolenga kuwafikisha watu kwa haraka katika maeneo mbalimbali, hususan hifadhi za taifa, maeneo ya milimani na sehemu zenye changamoto za kufikika kwa urahisi. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo, Afisa wa Udhibiti wa Ubora na Usalama wa kampuni hiyo, Julius Ngeno, amesema huduma wanazotoa zimebuniwa kwa lengo…