KAMATI YA UTAFITI YAPENDEKEZA MFUKO MAALUM KUINUA WACHIMBAJI WADOGO
KAMATI YA UTAFITI YAPENDEKEZA MFUKO MAALUM KUINUA WACHIMBAJI WADOGO Na John Bukuku – Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Utafiti wa Kuendeleza Wachimbaji Wadogo nchini Tanzania, Victor Tesha, amesema sekta ya madini inaendelea kuwa moja ya nguzo muhimu za mageuzi ya uchumi wa taifa kutokana na mchango wake katika ajira, mapato ya serikali, fedha za kigeni pamoja na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kamati hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, Tesha alisema mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa umeendelea kuongezeka kutoka asilimia 9.1 mwaka 2023 hadi zaidi ya asilimia 10 mwaka 2024 huku wastani wa asilimia 11.9 ukifikiwa kati ya Januari na Septemba 2025. Alisema mafanikio hayo yametokana na maboresho ya sera, usimamizi mzuri wa sekta pamoja na uwekezaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tesha alisema wachimbaji wadogo wana mchango mkubwa katika sekta hiyo kwani wanachangia t…