JESHI LA MAGEREZA LASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026

JESHI LA MAGEREZA LASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026
Na. Ssgt Mawazo Mtondo - Dodoma. Jeshi la Magereza kwa mara nyingine tena linashiriki kikamilifu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2026 Maadhimisho ambayo ni moja ya Maazimio ya Umoja wa Afrika (AU). Hivyo, Jeshi la Magereza linawakaribisha wananchi wote wa Tanzania kutembelea Banda la Magereza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma kuanzia Leo Juni 16 hadi 23, 2026. Maonesho hayo yatawakutanisha Wananchi, Taasisi za Umma na Wadau mbalimbali kwa lengo la kuelezea Dhima, Dira, Mafanikio, Changamoto zilizopo katika suala zima la urekebishaji Wafungwa, kutoa huduma na taarifa mbalimbali muhimu kuhusu shughuli zinazotolewa na Serikali kwa Wananchi kupitia Jeshi la Magereza na kuueleza Umma juu ya Mageuzi ya kisayansi yanayofanywa sasa na Jeshi katika uendeshaji na urekebishaji Wafungwa. Pamoja na kutoa huduma hizo, Jeshi la Magereza kupitia Maadhimisho haya linatoa elimu kw…