iTRUST YAFIKIA THAMANI YA BIL.176, YAWAKUTANISHA WAWEKEZAJI KATIKA MKUTANO MKUU
iTRUST YAFIKIA THAMANI YA BIL.176, YAWAKUTANISHA WAWEKEZAJI KATIKA MKUTANO MKUU Dar es Salaam, Tanzania – Juni 20, 2026 Kampuni ya iTrust Finance Limited imetangaza mafanikio makubwa baada ya thamani ya mali inayosimamiwa kufikia zaidi ya Shilingi bilioni 176, hatua inayotajwa kuwa ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika historia ya kampuni hiyo ya uwekezaji. Kwa mujibu wa taarifa ya fedha zilizokaguliwa kwa mwaka uliomalizika tarehe 31 Desemba 2025, mifuko mitano ya uwekezaji inayosimamiwa na iTrust imefikia thamani hiyo kupitia mifuko ya iCASH Fund, iSAVE Fund, iINCOME Fund, iGROWTH Fund na IMAAN Fund. Taarifa hiyo imeeleza kuwa thamani ya mali inayosimamiwa kwa kila mfuko ni pamoja na iCASH Fund Shilingi milioni 36,045, iSAVE Fund Shilingi milioni 10,656, iINCOME Fund Shilingi milioni 16,352, iGROWTH Fund Shilingi milioni 97,999 na IMAAN Fund Shilingi milioni 14,915. Mafanikio hayo yamewasilishwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanahisa (Annual General Meeting – AGM) wa mifuko hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam Juni 20, 2026, ukiwaleta pamoja wawekezaji kw…