INADES YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI 200 KISIMA CHA NDEGE SEKONDARI.
INADES YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI 200 KISIMA CHA NDEGE SEKONDARI.
Taasisi ya INADES Formation Tanzania imeadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti 200 ya kivuli na matunda katika Shule ya Sekondari Kisima cha Ndege iliyopo Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma. Zoezi hilo ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya “Panda Mti Tuilinde Kesho” iliyozinduliwa Januari 2026, yenye lengo la kuchangia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha utunzaji wa mazingira. Akizungumza baada ya shughuli ya upandaji miti iliyofanyika Juni 5, 2026, Mwakilishi wa INADES Formation Tanzania, Paul Ephras Chugu, amesema taasisi hiyo imefanikiwa kupanda miti zaidi ya 15,000 katika vijiji vinne vya Wilaya ya Bahi tangu kuanza kwa kampeni hiyo. Kwa upande wake, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Joyce Anania Jackson, ameipongeza INADES Formation Tanzania kwa ushirikiano mzuri unaoendelea kati ya taasisi hiyo na halmashauri katika kutekeleza shughuli za uhifadhi wa mazingira. Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisima cha Ndege, Mwalimu wa Mazingira …