EAC YATAKA SHERIA IMARA KULINDA WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII

EAC YATAKA SHERIA IMARA KULINDA WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII
Na Bora Fadhili, Arusha. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imezitaka serikali za nchi wanachama kuharakisha uundaji na uimarishaji wa sheria pamoja na sera madhubuti zitakazolinda watumiaji wa mitandao ya kijamii dhidi ya unyanyasaji wa kidijitali, huku wanawake na watoto wa kike wakitajwa kuwa miongoni mwa waathirika wakubwa wa matumizi mabaya ya teknolojia. Akizungumza Juni 26,2026 katika Kilele cha Kongamano la Pili la Mazungumzo ya Kizazi kwa Kizazi la Wanawake wa EAC, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake la Jumuiya hiyo, Fatuma Ndangiza, amesema matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yamechangia kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.  Amesema hali hiyo inahitaji hatua za haraka kutoka kwa serikali na mabunge ya nchi wanachama ili kuimarisha mifumo ya kisheria itakayowalinda watumiaji wa majukwaa ya kidijitali. Pia amesema ni muhimu kuongeza uwekezaji katika elimu ya usalama wa kidijitali, hasa kwa wanawake na wasichana, ili kuwajengea uwezo wa kutambua, kujiking…