DKT. SHEKALAGHE AWATAKA WATAALAMU KUSHIRIKIANA KULINDA MAFANIKIO YA AFYA YA UZAZI NDANI NA NJE YA MIPAKA YA TANZANIA

DKT. SHEKALAGHE AWATAKA WATAALAMU KUSHIRIKIANA KULINDA MAFANIKIO YA AFYA YA UZAZI NDANI NA NJE YA MIPAKA YA TANZANIA
Na Abdu Madenge, WAF – Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, amewataka wataalamu wa afya nchini kuendelea kushirikiana, kupeana nguvu na kubadilishana uzoefu ili kudumisha na kuendeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya afya, hususan katika eneo la afya ya uzazi, mama na mtoto. Dkt. Shekalaghe amesema hayo tarehe 13 Juni, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa Kikao cha Kamati ya Kitaalam (TWG 5) ya Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, ambapo alieleza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito. Hata hivyo, alionya kuwa mafanikio hayo yanaweza kupotea iwapo mshikamano, juhudi na afua zinazotekelezwa hazitasimamiwa ipasavyo. Katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ahmad Mohammed Makuwani, amesema kuwa kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa lengo la kupitia utekelezaji wa afua mbalimbali za…