DKT. SHEKALAGHE AWATAKA WADAU KUENDELEA KUUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA VIFO VYA MAMA NA MTOTO
DKT. SHEKALAGHE AWATAKA WADAU KUENDELEA KUUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA VIFO VYA MAMA NA MTOTO
Na Abdu Madenge, WAF – Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, ametoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha afya ya uzazi kwa kutoa msaada wa kifedha, kiufundi na rasilimali nyingine muhimu, huku akisisitiza dhamira ya Serikali ya kutokomeza au kupunguza kwa kiwango kikubwa vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika. Dkt. Shekalaghe amesema hayo tarehe 13 Juni, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akifunga Kikao cha Kamati ya Kitaalam (TWG 5) ya Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto. Akizungumzia umuhimu wa ushiriki wa wadau wa maendeleo, Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ahmad Mohammed Makuwani, amesema kikao hicho hufanyika kila robo mwaka kwa lengo la kuwaleta pamoja wataalamu na wadau wa maendeleo ili kupitia utekelezaji wa afua za afya ya uzazi, mama na mtoto na kujadili maeneo ya kipaumbele yatakayosaidia kufikia malengo ya mwaka wa fe…