DKT. MWIGULU: SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA SEKTA BINAFSI KATIKA KUINUA UBORA WA ELIMU NCHINI

DKT. MWIGULU: SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA SEKTA BINAFSI KATIKA KUINUA UBORA WA ELIMU NCHINI
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuthamini na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika sekta ya elimu kutokana na mchango wake mkubwa kwenye kuongeza ubora wa elimu na kuandaa rasilimali watu yenye maarifa, ujuzi na maadili yanayohitajika katika maendeleo ya Taifa. Dkt. Mwigulu amesema hayo alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 11 ya wahitimu wa Kidato cha Nne (Year 11–IGCSE) wa mwaka wa masomo 2025/2026 ya Shule ya Kimataifa ya Feza yaliyofanyika Salasala, Dar es Salaam, leo Ijumaa, Juni 12, 2026. "Nimekuja leo kwa kuwa Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambua ubia huu muhimu ambao shule yenu imekuwa ikifanya katika sekta ya elimu. Hatuwezi kuyataja mafanikio katika sekta ya elimu bila kutaja mchango wa shule za sekta binafsi, na kwa umuhususi shule za Feza," amesema Dkt. Mwigulu. Amesema Taasisi ya Feza ni miongoni mwa taasisi zilizochangia kwa kiasi kikubwa mageuzi ya elim…