DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI LA JENGO LA TAALUMA TIA SINGIDA
DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI LA JENGO LA TAALUMA TIA SINGIDA WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika elimu ya juu kwa kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia ili kuandaa rasilimali watu yenye ujuzi na uwezo wa kuchangia maendeleo ya Taifa. Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 27, 2026) alipoweka jiwe la msingi la Jengo la Taaluma la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Singida. Waziri Mkuu amesema ujenzi wa jengo hilo unaakisi dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuboresha mazingira ya elimu ya juu na kusogeza huduma hizo karibu na wananchi. “Leo hii jengo hili la chuo chetu liko Singida. Hii ni hatua kubwa sana. Hongereni bodi, hongereni chuo, hongereni wanafunzi. Tunawatakia kila la heri,” amesema. Aidha, amewapongeza wahandisi, washauri na wakandarasi wazawa wanaotekeleza mradi huo akisema ushiriki wao unaonesha uwezo wa Watanzania katika kutekeleza miradi mikubwa …