DKT. MWIGULU AAGIZA UCHUNGUZI WA MAPATO YA MAEGESHO IFUNDA

DKT. MWIGULU AAGIZA UCHUNGUZI WA MAPATO YA MAEGESHO IFUNDA
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ukusanyaji wa mapato ya maegesho katika eneo la Ifunda wilayani Iringa na kuwasilisha taarifa kamili kuhusu namna mapato hayo yalivyokuwa yakikusanywa kabla na baada ya mabadiliko ya mfumo wa ukusanyaji pamoja na matumizi yake. Ametoa agizo hilo leo Jumamosi, Juni 6, 2026 wakati akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo la Kalenga katika mkutano wa hadhara uliofanyika Ifunda wilayani Iringa mkoani Iringa. Agizo hilo lilitolewa baada ya Waziri Mkuu kuwataka viongozi wa TANROADS, Halmashauri na TAKUKURU kutoa maelezo kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya maegesho katika eneo hilo na mabadiliko yaliyofanyika katika usimamizi wake. “Nataka ripoti yote ya zoezi la ukusanyaji jinsi ambavyo limefanyika, kabla na sasa. Nataka tujue fedha hizi zimeenda wapi na wahusika walikuwa nani,” alisema Dkt. Mwigulu. Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kupitia mifumo ya uwaji…