DKT. KIJAJI: NYUMBA ZA IBADA ZIWE CHANZO CHA MSHIKAMANO NA AMANI KWA TAIFA

DKT. KIJAJI: NYUMBA ZA IBADA ZIWE CHANZO CHA MSHIKAMANO NA AMANI KWA TAIFA
KONDOA, DODOMA Mbunge wa Jimbo la Kondoa ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amesisitiza kuwa nyumba za ibada zinapaswa kuwa sehemu ya kuimarisha mshikamano, umoja na amani miongoni mwa wananchi na si kuwa chanzo cha migawanyiko katika jamii. Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua rasmi Msikiti wa Filimo uliopo Kata ya Mnenia, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Kijaji amesema kuwa nyumba za ibada zina nafasi kubwa katika kujenga maadili mema, kuimarisha upendo na kukuza mshikamano wa kijamii, hivyo zinapaswa kutumika kwa malengo hayo kwa manufaa ya Taifa. “Msikiti huu uwe chachu ya mshikamano ndani ya jamii yetu. Nawapongeza viongozi wa dini kwa kusimama katika haki na kuendelea kuhubiri amani na umoja miongoni mwa wananchi,” alisema Dkt. Kijaji. Aidha, aliongeza kuwa kila mtu ana wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu katika jamii na mbele za Mungu, akibainisha kuwa maendeleo y…