DKT. DUGANGE: SERIKALI KUIMARISHA MTANDAO WA BARABARA NEWALA VIJIJINI

Na Timothy – Mwakyenda – MAELEZO. Serikali imeahidi kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika Jimbo la Newala Vijijini mkoani Mtwara kwa kutenga fedha za matengenezo na kutoa maelekezo kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha barabara zilizoharibiwa na mvua zinakarabatiwa kwa haraka ili kurejesha mawasiliano na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa bungeni – Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Newala Vijijini, Dkt. Yahaya Ismail Nawanda, ambaye alitaka kufahamu ni lini Serikali itajenga Barabara ya Mkoma One–Mnyambe–Miyuyu inayotegemewa na wananchi wa eneo hilo. Dkt. Dugange amesema Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa matengenezo na uboreshaji wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 37, ambayo ina umuhimu mkubwa katika kuwaunganisha wananchi na huduma muhimu za kijamii, ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Ndanda. Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha …