CHUO CHA UHASIBU ARUSHA IAA KUKUTANISHA WADAU WA UTALII KUTOKA MATAIFA MBALI MBALI,KUELEKEA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA NNE LA UTALII.
CHUO CHA UHASIBU ARUSHA IAA KUKUTANISHA WADAU WA UTALII KUTOKA MATAIFA MBALI MBALI,KUELEKEA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA NNE LA UTALII.
Na Ashura Mohamed, ARUSHA. Naibu Mkuu wa Chuo, Upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha IAA, Dkt. Grace Temba, ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya maandalizi ya kongamano la kimataifa la utalii linalotarajiwa kufanyika tarehe 25 Septemba, 2026 mkoani Arusha. Tukio hilo la kongamano ni muhimu kwa taasisi hiyo na maalum kwa wadau wa utalii kutoka maeneo mbali mbali duniani likilenga wadau wa sekta ya utalii kwa dhima kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani ili kuendelea kuhamasisha idadi ya watalii kuongezeka. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Dkt. Grace amesema kuwa lengo hasa ni kuhakikisha wadau mbali mbali wanashiriki na kufanya kongamano hilo kujumlisha watunga sera, wadau wa utalii kutoka ndani na nje ya nchi kujiandaa na kushiriki kwa ufanisi zaidi. “Siku ya kongamano tunawaweka pamoja wadau mbali mbali tunatoa taarifa mbali mbali za utafiti zilizofanywa na wadau mbali mbali waliopo katika sekta ya utalii lakini pia Chuo cha Uhasibu Arusha, …