BILIONI 51 ZATUMIKA KUBORESHA UWANJA WA NDEGE KIGOMA – PROF. MBARAWA
BILIONI 51 ZATUMIKA KUBORESHA UWANJA WA NDEGE KIGOMA – PROF. MBARAWA
Na mwandishi wetu,Kigoma Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imetumia shilingi bilioni 51 kuboresha Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, huku utekelezaji wa mradi huo ukiwa umefikia asilimia 67 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba au Novemba 2026 Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo mkoani Kigoma, leo tarehe 25 Juni, 2026 Prof. Mbarawa amesema jengo jipya la abiria litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria laki nne kwa mwaka na kupokea abiria 500 kwa wakati mmoja, hatua itakayoongeza ufanisi wa huduma za usafiri wa anga katika ukanda huo Ameongeza kuwa mradi huo utaiwezesha Kigoma kuwa na uwanja wa ndege wenye uwezo wa kutoa huduma mchana na usiku kutokana na uwekaji wa mifumo ya taa za kuongozea ndege Aidha, amesema Serikali ina mpango wa kuongeza urefu wa njia ya kurukia na kutua ndege ili kuruhusu ndege kubwa zaidi kutumia uwanja huo Prof. Mbarawa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kukamilika kwa mradi huo ambao ulikuwa umekwama kwa m…