Balozi wa Uganda Kuandaa Mkutano wa Viongozi wa Habari Kuharakisha Umoja wa Afrika Mashariki
Balozi wa Uganda Kuandaa Mkutano wa Viongozi wa Habari Kuharakisha Umoja wa Afrika Mashariki
Na Mwandishi wetu, TBN, Dar es salaam Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Kanali Mstaafu Fred Mwesigye, ametangaza kuandaa kikao maalumu kitakachowakutanisha viongozi wa Baraza la Habari Afrika Mashariki chini ya uenyekiti wa David Omwoyo, Mtendaji Mkuu wa Baraza la Habari Kenya kujadili mikakati ya kuendeleza utalii wa kiutamaduni, uchumi wa ubunifu na sekta ya michezo inayokua kwa kasi katika ukanda huu. Hatua hiyo inafuatia kikao cha ngazi ya juu kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilichowakutanisha Balozi Mwesigye, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Ernest Sungura, pamoja na wawakilishi wa Umoja Conservation Trust (UCT) wakiongozwa na Bryan Toshi , ambacho kilijadili kwa kina nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Shirikisho la Afrika Mashariki na kuharakisha umoja wa kikanda. Katika kikao hicho, washiriki walikubaliana kwamba tasnia ya habari katika Afrika Mashariki inapaswa kuondokana na mtazamo wa kuripoti matukio ya kitaifa kwa namna ya kujitenga, na badala y…