BALOZI OMAR NA MKURUGENZI MPYA WA AFRIEXIM BANK WATETA DAR ES SALAAM
BALOZI OMAR NA MKURUGENZI MPYA WA AFRIEXIM BANK WATETA DAR ES SALAAM
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mpya wa Benki ya Afrexim Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Humphrey Nwugo, aliyefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni, akiambatana na wajumbe wengine wa benki hiyo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo alitumia fursa hiyo kuelezea umuhimu wa ushirikiano imara, mitaji ya muda mrefu na mbinu bunifu za ufadhili kati ya Benki hiyo na Serikali ya Tanzania ili kufikia azma ya kuwa uchumi wa dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050. Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam WAZIRI wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema Tanzania inaiona Benki ya Afrexim kama mshirika wa kimkakati katika safari ya mageuzi ya kiuchumi ya nchi, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano imara, mitaji ya muda mrefu na mbinu bunifu za ufadhili ili kufikia azma ya kuwa uchumi wa dola trilioni moja if…