AWAMU YA NNE YA TUZO ZA WATAFITI YAFUNGULIWA, BILIONI 1.5 ZIMETENGWA

AWAMU YA NNE YA TUZO ZA WATAFITI YAFUNGULIWA, BILIONI 1.5 ZIMETENGWA
Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Dodoma  Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefungua rasmi dirisha la Awamu ya Nne ya Tuzo kwa watafiti na wahadhiri wanaochapisha matokeo ya tafiti katika majarida yenye hadhi ya juu kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari Juni 18, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema dirisha hilo litakuwa wazi kuanzia Juni 19 hadi Oktoba 31, 2026, likilenga kutoa fursa kwa watafiti kuwasilisha machapisho yao kwa ajili ya ushindani wa tuzo hizo. Amesema tuzo hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuhamasisha utafiti na ubunifu wa ndani, kupunguza utegemezi wa teknolojia kutoka nje, pamoja na kuimarisha mchango wa sayansi na teknolojia katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Aidha ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027, serikali imetenga Shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuimarisha utekelezaji wa tuzo hiyo, ikiwa ni motisha kwa watafiti kufanya tafiti zenye ubora na zinazotoa suluh…