ALBINISM SPORTS CLUB NA TASACI WASHIRIKIANA KUANDAA MECHI YA KIRAFIKI NA TIMU YA BUNGE ITAKAYOCHEZWA JUNI 6

ALBINISM SPORTS CLUB NA TASACI WASHIRIKIANA KUANDAA MECHI YA KIRAFIKI NA TIMU YA BUNGE ITAKAYOCHEZWA JUNI 6
ALBINISM Sports Club yenye Makao Makuu yake jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TASACI), imeandaa mechi ya kirafiki kati ya timu ya Bunge. Mechi hiyo ya kirafiki itakayofanyika Juni 6 2026 katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma na mtanange huo huo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuongeza Uelewa kuhusu Ualbino, ambayo huadhimishwa duniani kote Juni 13 Juni kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha jamii kuhusu haki, usawa, heshima na ustawi wa watu wenye ualbino. Taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari leo Juni 3,2026 na Abdallah Majiwa ambaye ni Mwenyekiti wa Albinism Sports Club amesema tukio hilo linatarajiwa kuwakutanisha pamoja Wabunge, watu wenye ualbino, wananchi wa Jiji la Dodoma na maeneo ya jirani na wadau mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu. Amefafanua kuwa kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Wezesha Watu Wenye Ualbino kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu.” Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa…