AGIZO LA SERIKALI LAMPA TUMAINI JOSEPH MTEI, AWAHIMIZA WAZAZI KUTOWAFICHA WENYE ULEMAVU.
AGIZO LA SERIKALI LAMPA TUMAINI JOSEPH MTEI, AWAHIMIZA WAZAZI KUTOWAFICHA WENYE ULEMAVU.
Kijana Joseph Mtei mwenye mahitaji maalum ambaye kwa sasa anafanya kazi katika kampuni tangu ya UJUZI katika kiwanda cha kutengeneza samani cha VETA Dodoma, amepongeza uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kumuwezesha kupata ajira rasmi. Agizo hilo lilitolewa Juni 23, 2026, wakati wa kilele cha wiki ya utumishi wa umma Jijini Dodoma na Waziri wa TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, ambaye alimwelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora, kuhakikisha Joseph Mtei anapatiwa ajira rasmi, amesema hatua hiyo imeonyesha kuwa serikali inatambua uwezo wa watu wenye ulemavu na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya taifa. Akizungumza katika mahojiano maalum na Michuzi TV Juni 24, 2026, jijini Dodoma, Mtei alisema safari yake ya maisha imekuwa ya changamoto nyingi tangu utotoni na licha ya kuzaliwa bila mikono lakini hakukata tamaa, Ameeleza kuwa elimu na mafunzo ya ufundi vimemwezesha kujijengea uwezo wa kufanya kazi na kujitegemea kama ilivyo kwa watu w…